TADB YATUNUKIWA TUZO YA TAASISI YA FEDHA KINARA KATIKA KUWEZESHA MIRADI YA UFUGAJI WA KUKU TANZANIA

****

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetunukiwa tuzo ya kuwa Taasisi ya Fedha Kinara katika Kuwezesha miradi ya ufugaji wa Kuku nchini, katika Maonesho ya Kumi ya Ndege Wafugwao (Tanzania Poultry Show 2026).

Tuzo hii ilitolewa kwa kutambua mchango wa TADB katika kuwawezesha wadau wa sekta ya kuku kupitia huduma za kifedha zinazochochea uzalishaji, ukuaji wa biashara na maendeleo ya uchumi wa Tanzania.

TADB inaendelea kujizatiti kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi, kuimarisha mnyororo wa thamani wa kilimo, mifugo na uvuvi, na kuchangia maendeleo endelevu ya sekta ya kilimo nchini.

Maonesho haya yamefanyika tarehe 16 na 17 Oktoba 2026 katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

TADB – Kilimo Kinabenkika

 #TanzaniaPoultryShow2026

#WizarayaMifugo
 

0/Post a Comment/Comments