TADB YAWAWEZESHA WATEJA 14 KUONA KILIMO CHA KISASA JAPAN

 

********

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewawezesha wateja wake 14 kwenda nchini Japan kushiriki maonesho ya J-AGRI Tokyo, yanayohusisha teknolojia na ubunifu mbalimbali katika sekta ya kilimo.

 Ziara hiyo imefanyika wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, ikiwa na lengo la kuwapa washiriki nafasi ya kujifunza teknolojia zinazoweza kuboresha uzalishaji, usindikaji, uhifadhi na uongezaji thamani wa mazao.

 Katika maonesho hayo, wateja hao watapata fursa ya kuona mashine za kilimo, mifumo ya umwagiliaji, kilimo janja, drones pamoja na teknolojia za kuhifadhi na kusafirisha mazao.

 Aidha, watakutana na wazalishaji na wasambazaji wa vifaa vya kilimo kutoka Japan, huku wakitafuta teknolojia zinazoweza kuendana na mahitaji ya wakulima na wafanyabiashara wa kilimo nchini Tanzania.

 Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Frank Nyabundege, Akimzungumza na Waandishi WA habari Mapema leo jijini Dar es salaam, amesema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya benki kwenda zaidi ya kutoa mikopo kwa kuwapatia wateja wake maarifa, teknolojia na uzoefu wa kimataifa.

 Nyabundege amesema mpango huo unaendana na kaulimbiu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ya mwaka huu, “The Extra Mile" inayosisitiza umuhimu wa kwenda hatua ya ziada katika kuwahudumia wateja.

 Kwa upande wake, mwakilishi wa wateja hao, Kamal Simba, ameshukuru TADB kwa fursa hiyo, akisema wanatarajia kurejea nchini na maarifa na uzoefu watakaoutumia kuboresha shughuli zao.

 Wateja hao 14, wanaojihusisha na usindikaji, maghala, ununuzi wa mazao, mitambo, pembejeo na umwagiliaji, wamewezeshwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 62 na sasa wanatarajiwa kutumia fursa hiyo kujifunza teknolojia zitakazoongeza tija katika shughuli zao









0/Post a Comment/Comments