******
Na Mwandishi wetu.
Dodoma.
Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini TIRA kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Bima wamechangia jumla ya ya shilingi Mil.221 katika Hospitali ya Benjamini Mkapa BMH kwa lengo la kusaidia kugharamia kusaidia matibabu ya upandikizaji uloto kwa watoto wenye ugonjwa wa selimundu (sickle cell) na upandikizaji wa figo kwa wananchi wenye uhitaji.
Akikabidhi hundi ya mchango huo kwa mkurugenzi mtendaji wa Hospitali hiyo, kamishina wa Bima nchini Dkt.Baghayo Saqware ameupongeza uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa ubunifu wa kuanzisha mfuko maalum unaouwezesha wadau mbalimbali kuchangia fedha za kusaidia matibabu ya figo na uloto na kuahidi TIRA kuendelea kushiriki kuchangia.
"Mchango huu kiasi hiki Cha fedha ni fedha zilizotoka mifukoni mwa wafanyakazi wa TIRA pamoja na wadau wetu wa sekta ya bima ambao kwa pamoja tumeweza kuchangishana kiasi hiki Cha fedha na tutaendelea kuiunga mkono Hospitali hii ya Benjamini katika kusaidia matibabu ya afya kwa watanzania walio na changamoto kama hizi" Alisema Dkt.Saqware.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo Cha mahusiano wa mamlaka hiyo TIRA Bi.Hadija Maulidi amesema kuwa mchango huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha afya za watanzania hususani kusaidia watoto wadogo wenye changamoto za ugonjwa wa selimundu na figo ambapo kwa kufanya hivyo inaonesha kwa namna sekta ya bima inavyojali afya za watanzania.
Nae mkurugenzi Mtendaji wa sekta ya bima ya Metro Bw.Amani Boma akiwakilisha wadau wa sekta ya Bima amesema kuwa moto wa kampuni yao unatoa msisitizo wa kwenda pamoja na jamii na kufika mbali na kufanya makubwa zaidi kwa jamii(Together we will and go extra miles).
Aidha kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bima ya Sanlam Allianz Bw.Jukius Magabe amesema kampuni za bima zinaamini katika kurudisha kwa jamii kutoka kwenye kile kinachopatikana na kuahidi kuendelea kuiunga mkono serikali na Hospitali hiyo ya Benjamini Mkapa.
Akitoa neno la shukrani Mkurugenzi Mtendaji wa wa Hospitali hiyo ya Benjamini Mkapa Profesa Abel Makubi amesema kuwa wadau wa bima wamefanya jambo jema na kubwa la kiutu hali inaonesha kuguswa na matatizo ya jamii na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika kupandikiza uloto na figo kwa wenye uhitaji.

Post a Comment