TRA YAKUSANYA SHILINGI TRILIONI 10.65, YAVUKA LENGO KWA ASILIMIA 107.49


******

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Shilingi trilioni 10.65 katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2026, sawa na asilimia 107.49 ya lengo la Shilingi trilioni 9.91 kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/27.

Kwa mujibu wa taarifa ya utendaji kazi ya TRA iliyotolewa Oktoba 1, 2026, makusanyo hayo yameongezeka kwa asilimia 18.81 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 8.96 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha 2025/26.

Katika mwezi Julai 2026, TRA ilikusanya Shilingi trilioni 3.25, sawa na asilimia 109.21 ya lengo la Shilingi trilioni 2.97.

Mwezi Agosti, TRA ilikusanya Shilingi trilioni 3.22 dhidi ya lengo la Shilingi trilioni 2.97, sawa na asilimia 108.16.

Kwa upande wa Septemba, mamlaka hiyo ilikusanya Shilingi trilioni 4.19, sawa na asilimia 105.71 ya lengo la Shilingi trilioni 3.96.

TRA imesema mafanikio hayo yametokana na kuendelea kuboresha mifumo, mazingira ya ufanyaji biashara na utoaji wa huduma kwa walipakodi, hatua zinazolenga kurahisisha na kuchochea ulipaji wa kodi kwa hiari.

Aidha, TRA imesema imeendelea kudhibiti vitendo vya ukwepaji kodi na kuimarisha mahusiano ya kiutendaji na wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, hatua hizo zimechangia kuendelea kuvuka malengo ya makusanyo na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.



0/Post a Comment/Comments