Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Jukwaa Uhifadhi wa Wanyamapori Barani Afrika (24th African Wildlife Consultanive Forum - 24 AWCF) wametoka na maazimio 10 yenye leongo la kuimarisha Uhifadhi Wanyamapori na matumizi endelevu kwa maslahi mapana ya wananchi.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Mkutano huo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wanyamapori nchini Dkt. Alexander Lobora, alipokuwa akifunga rasmi Mkutano huo kwa kimataifa, amesema, Jijini Arusha
Dkt. Lobora amesema kuwa mkutano huo umekuwa wa mafanikio makubwa na kuwa maazimio yaliyowekwa yatatekelezwa na kila nchini washiriki ndani ya mwaka moja na utekelezaji huo kupimwa kwenye mkutano ujao wa 25.
"Msingi wa Mkutano huo ilikuwa ni kujadili kuhusu uhifadhi wa Wanyamapori, Matumizi endelevu na namna sekta ya Wanyamapori inavyoweza kuchangia zaidi maendeleo ya jamii zinazo zunguka maeneo ya hifadhi katika Bara yetu la Afrika". Alisema Dkt. Lobora.
Ameongeza kuwa pamoja na mkutano huo, washiriki walipata nafasi ya kutalii kwenye Eneo la Hifadhi ya Ngorongo hali iliyo pelekea kutamani kurudi tena nchini na familia zao.
Naye Bi. Jeanette Selier kutoka Afrika Kusini, amesema mkutano huo kufanyikia Tanzania umewapa nafasi adhimu ya kujifunza mengi hasa namna Wizara ya Maliasili na Utalii inavyo shirikisha jamii kwenye uhifadhi wa Wanyamapori.










Post a Comment