FCC YATWAA TUZO YA UBORA YA AFRIKA MASHARIKI 2026, YATAMBULIWA KAMA TAASISI BORA YA UMMA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA.

********

Tume ya Ushindani (FCC) ya Tanzania imeibuka mshindi wa jumla katika kipengele cha Ubora wa Huduma kwa Taasisi za Umma katika Tuzo za Ubora za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Regional Quality Awards 2026), zilizofanyika usiku wa tarehe 2 Novemba 2026 katika Hoteli ya Movenpick jijini Kigali, nchini Rwanda.

Tuzo hiyo ni kutambua dhamira na juhudi za FCC katika kutoa huduma bora kwa Umma, kusimamia masoko kwa ufanisi, kulinda walaji na kuendeleza ushindani wa haki.

 Mafanikio hayo yanaifanya FCC kuwa miongoni mwa Taasisi za Umma zinazotambuliwa katika kuimarisha utamaduni wa ubora wa huduma ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

FCC imeshika nafasi ya kwanza katika kipengele hicho kupitia huduma zake za Usimamizi wa Masoko na Ushindani wa Haki, ikiibuka mshindi dhidi ya Taasisi nyingine zilizokuwa zimeingia katika kinyang'anyiro hicho kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Taasisi hizo ni Kenya Electricity Generating Company PLC ya Kenya, iliyowasilisha huduma za uzalishaji wa umeme kwa kiwango kikubwa (Large-Scale Electricity Generation); Rwanda Meteorology Agency ya Rwanda, kupitia huduma za utabiri wa hali ya hewa (Weather Forecasting); pamoja na National Identification and Registration Authority (NIRA) ya Somalia, kupitia huduma za utambuzi wa utambulisho wa taifa (National Identification Services).



 

0/Post a Comment/Comments