NIDHAMU, UBUNIFU NGUZO ZA MAFANIKIO – SANJAY RAJA

*****

Mafanikio katika shughuli za kibiashara hayaji kwa ndoto pekee, bali yanahitaji kujituma, nidhamu ya uwajibikaji, udadisi na kumweka MUNGU mbele katika shughuli za kila siku.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya huduma za kimtandao, Sanjay Raja, baada ya kampuni yake kutunukiwa tuzo ya utoaji huduma bora kwa wateja mwaka 2026, zilizotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Raja amesema kampuni hiyo imekuwa ikitoa huduma kwa kipindi cha miaka 25, jambo lililoiwezesha kupata uzoefu na ujuzi wa kutosha katika kubuni mbinu mpya za kuwahudumia wateja na kuendana na mabadiliko ya teknolojia ili kujenga uaminifu na kuwafanya wateja waendelee kudumu.
 

0/Post a Comment/Comments