TPF MKOA WA DAR YAJIZATITI KUFANYA MIRADI YA KIMAENDELEO

Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Peace Family (TPF) Mkoa wa Dar es salaam  Khamis Salehe akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha TPF kilichofanyika katika Viwanja vya sabasaba maonyesho jijini Dar es salaam tar 28 novemba 2026 
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Peace Family (TPF) Mkoa wa Dar es salaam  Elizabeth Sheyo akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha TPF kilichofanyika katika Viwanja vya sabasaba maonyesho jijini Dar es salaam tar 28 novemba 2026.
Baadhi ya wanachana na viongozi wa Taasisi ya Tanzania Peace Family (TPF) Mkoa wa Dar es salaam  Elizabeth Sheyo walioshiriki kwenye kikao cha kawaida cha TPF kilichofanyika katika Viwanja vya sabasaba maonyesho jijini Dar es salaam tar 28 novemba 2026.
.....................

NA MUSSA KHALID 

Taasisi ya Tanzania Peace Family (TPF) Mkoa wa Dar es salaam imeendelea kuwasisitiza wanachama wake wakiwemo viongozi wa mkoa kuendelea kudumisha umoja na mshikamano ili kuijenga taasisi hiyo kuwa imara na kutekeleza kwa wakati malengo iliyojiwekea. 

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa TPF Mkoa wa Dar es salaam Khamis Salehe wakati akizungumza kwenye kikao cha kawaidia cha TPF kilichofanyika katika Viwanja vya sabasaba maonyesho jijini Dar es salaam tar 28 novemba 2026  

Salehe amesema kuwa mkoa huo umejiwekea mipango mingi ya kuinufaisha Taasisi hiyo hivyo amewasisitiza viongozi kuhakikisha wanahudhuria vikao mara kwa mara ili kujadili mambo mbalimbali yatakayosaidia kuyafikia mafanikio. 

"Hii ni taasisi inayojishughulisha na amani hivyo ni lazima kuwe na umoja na mshikamano ili kuijenga taasisi hii kuwa imara nyakati zote"amesema Mwenyekiti Salehe 

Awali akizungumza Katibu Mtendaji wa TPF Mkoa wa Dar es salaam Elizabeth Sheyo amewasisitiza wanachama kuhakikisha wanatumia fursa pindi zinapojitokeza huku akiwasihi kukamilisha  kwa wakati madeni wanayodaiwa ili taasisi iendeleze mipango yako vizuri ikiwemo miradi mbalimbali ambayo inatarajiwa kutekelezwa. 

Elizabeth amesema kuwa kwa sasa wameendelea kuitekeleza miradi ikiwemo ya utoaji wa elimu katika Vyuo,Shule na maeneo mbalimbali ili wanafunzi wafahamu elimu ya uzalendo na amani kwa nchi yao. 

"Tunaendelea na mipango ya kufanya mradi wa kutoa elimu lakini tayari tunafursa wizara ya madini kwa maana uchimbaji wa madini  ambapo tunatakiwa iombwe leseni ya uchimbaji wa madini na Kokomo na hata mchanga yote haya tunayafanya kwa lengo la kuiimarisha taasisi iweze kujiendeleshq kwa ufanisi mzuri"amesema Katibu Sheyo 

Aidha ameeleza kuwa kwa sasa watahakikisha wanakwenda sambamba na  wananchama wanaokwenda sawa na malengo ya taasisi ikiwemo kulipa kiingilio na ada kwa wakati kwani ndio msingi bora kwa kufanilisha mipango yao. 

Kuhusu suala la Vitambulisho kwa wanachama Katibu Elizabeth amewaahidi kuwa vipo tayari na wapo kwenye mpango wa kuandaa siku maalum ya kuvigawa ambapo vitakuwa kwenye Idari ya Itifaki na usalama Mkoa na kila mmoja aliyekidhi vigezo atapatiwa.

0/Post a Comment/Comments