TUMIENI MEWAKA KATIKA KUFUNDISHANA MBINU ZA JOLLY PHONICS - DKT. KOMBA


 *****

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba ametoa wito kwa walimu wanao shiriki mafunzo ya mbinu za ufundishaji wa somo la Kiingereza (Jolly Phonics) kutumia MEWAKA zao ili kuwafundisha walimu ambao hawajapata fursa ya kushiriki mafunzo hayo.

Ametoa wito huo kwa njia ya darasa janja (smart class) leo Novemba 23, 2026 wakati akifungua mafunzo hayo yanayotarajia kufanyika katikati mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Ruvuma na Lindi ili kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa lugha ya kiingereza.

Dkt. Komba amesema, mafunzo hayo yatasaidia kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiingereza huku, akiwahimiza walimu kufuatilia mafunzo kwa makini na kuomba ufafanuzi wa ziada pindi itapohitajika.

“Naomba sana mfuatilie kwa makini mafunzo haya ili muweze kupata ujuzi utakaowasaidia kuwafundisha wanafunzi katika madarasa yenu. Hakikisheni mnajifunza vizuri ili msaidie wanafunzi wenu kuelewa zaidi,” amesema Dkt. Komba.

Poa, Dkt. Komba amewashukuru Jolly Futures kwa kushirikiana na TET katika kutoa mafunzo hayo, yanayoendeshwa kwa mfumo wa darasa janja, huku wakufunzi wa TET na Jolly Futures wakiwasaidia walimu ana kwa ana.

Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo Bi. Sheba Moyo amesema kuwa, mafunzo hayo ni muhimu kwa walimu ambapo itasaidia wanafunzi shuleni kuelewa zaidi somo la kiingereza na kuwataka walimu hao waendelee kujifunza zaidi kupitia jumuiya zao za ujifunzaji kama vile MEWAKA.

Mafunzo yameanza katika Mkoa wa Dar es Salaam na yataendelea katika mikoa ya Lindi, Ruvuma na Mbeya.










0/Post a Comment/Comments