UTAFITI WABAINI CHANGAMOTO ZA WALIMU, KULENGA KUBORESHA ELIMU


 *****

Wataalamu wa elimu kutoka Tanzania, Kenya na Sudan Kusini wamekutana katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Elimu (DUCE), jijini Dar es Salaam, kujadili utafiti unaolenga kubaini changamoto zinazowakabili walimu na kutafuta njia za kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.

Utafiti huo unaotekelezwa kupitia Mpango wa Kuimarisha Maendeleo ya Kitaaluma na Ushauri kwa Walimu (SITI), unalenga kuimarisha uwezo wa walimu na kuboresha matokeo ya kitaaluma kwa wanafunzi.

Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Abdu Maulid, amesema matokeo ya utafiti huo yatasaidia kuongeza maarifa ya walimu na kuweka mazingira bora ya ufundishaji.

Amesema kuboresha uwezo wa walimu ni hatua muhimu katika kuongeza uelewa wa wanafunzi na kuinua kiwango cha ufaulu.

Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Elimu (DUCE), Profesa Mshiriki Florensi Kyaruzi.

Naye Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Elimu (DUCE), Profesa Mshiriki Florensi Kyaruzi, amesema utafiti huo umechochewa na changamoto zilizobainika kwa walimu katika masomo yaliyofanyiwa utafiti.

Amesema kupitia utafiti huo, wataalamu wanatarajia kutoa mapendekezo yatakayosaidia kutatua changamoto hizo na kuboresha mbinu za ufundishaji.

Kwa upande wao, walimu walioshiriki katika utafiti huo wamesema mradi huo utawasaidia kuboresha namna wanavyofundisha na kuongeza ufanisi katika kuwafundisha wanafunzi.





















0/Post a Comment/Comments