Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema zaidi ya asilimia 85 ya Watanzania sasa wanapata huduma za afya ndani ya umbali wa kilometa tano kutoka maeneo wanayoishi, kufuatia ongezeko la vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Serikali imeongeza vituo vya afya na zahanati na kufikia 13,683, huku hospitali za wilaya zikiongezeka na kufikia 194 mwaka 2025.
Aidha, hospitali za rufaa za mikoa zimeongezeka kutoka 21 hadi 28, huku hospitali za taifa na kanda maalumu zikiwa 13.
Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamisi, Novemba 26, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Kisayansi wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto Mchanga, Mtoto, Vijana na Lishe.
Ameongeza kuwa, wodi maalumu za watoto wachanga zimeongezeka kutoka 14 mwaka 2018 hadi kufikia 438 mwaka 2025, hatua inayolenga kuboresha huduma kwa watoto wanaohitaji uangalizi maalumu.
Amesema upanuzi huo wa miundombinu ya afya umeongeza fursa za wananchi kupata huduma karibu na maeneo yao, mijini na vijijini.
Rais Samia amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma za afya nchini.

Post a Comment