TAASISI YA TDSP YAENDELEA KUWAWEZESHA WAKULIMA KUWEZA KUJIKWAMUA KIUCHUMI.



Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika linalojishughulisha na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi TDSP Athuman Mbonde akitoa maelekezo ya namna mradi huo utakavyofanyika katika kijiji hicho.

Diwani wa Kata ya Mwarusembe Rashid Ally akizungumza na amepongeza Uwekezaji huo kusema utaongeza fursa kwa wananchi.

Baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza katika hafla hiyo

................................................... 

NA MUSSA KHALID,PWANI 

Takriban vikundi 10 vya wadau wa kilimo pamoja na wananchi wa kawaida zaidi ya 7 wanataraji kufanya Uwekezaji wa kulima zao la Pilipili Kichaa katika shamba lenye ukubwa wa Hekari 100 lililopo kijiji cha Bigwa eneo la Mtikatika Kata ya Mwarusembe Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa kilimo Cha Pilipili katika eneo hilo,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika linalojishughulisha na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi TDSP Athuman Mbonde amesema wameamua kujikitia katika kilimo cha Pilipili kichaa kwani huo ni muendelezo wa Taasisi yao kuendelea kuwasaidia wakulima waweze kujikwamua kiuchumi wakiunga mkono serikali katika adhma ya kuwasaidia watanzania kuwa na maisha bora.

Mr Mbonde amesema eneo hilo wamelikodisha kwa mkataba wa miaka 20 ili kuweza kuliendeleza na kuleta fursa kwa watu wa Mkuranga na maeneo ya jirani na kueleza kuwa wameamua kwenda kuwekeza katika kijiji hicho kutokana na udongo wake kuwa na rutuba lakini pia maji yake ni ya uhakika.

‘Kwa sasa nina Program ya kuwezesha vijana wanawake na watu wenye hali duni hususani katika program ya kilimo Mkataba ambapo eneo hili tumepata mdau na tumekodi kwake ili kuweza kuliendeleza ili kuweza kuwanufaisha wakulima’amesema Mr Mbonde

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mwarusembe Rashid Ally amepongeza Uwekezaji huo kusema utaongeza fursa kwa wananchi kunufaika huku akiwataka waendele kufata taratibu kwa ngazi zote za serikali  ikiwemo Wilaya ili waweze kutambulika jambo litakalosaidia kufanikisha mradi huo kwa ubora pasipo changamoto za aina yeyote. 

Kwa upande wao baadhi ya wakulima wamesema malengo yao ni kuhakikisha wanafanya kilimo hicho chenye tija kwani wamebaini kina manufaa makubwa kutokana na mauzo yake Kilo Pilipili Kichaa kuwa Sh.6500 kwa baadhi ya wanunuzi.

Naye Mwwnyekiti wa Mtandao wa wakulima Wilaya ya Mkuranga (MVIWATA) Kudra Msumi ameipongeza Taasisi hiyo ya TDSP kwa kuonyesha nia ya kuwasaidia wakulima wa Tanzania kuweza kujikwamua kupitia miradi mbalimbali ukiwemo huo wa Pilipili kichaa.

Katika hafla hiyo TDSP wameambata na Mnunuzi wa Pilipili Kichaa Mkama Phumbwe kutoka Taasisi ya Sunset Agribusiness pamoja na waagizaji wa mbolea za Organic na wasambazaji Tanzania ambapo wamewaeleza wakulima taratibu mbalimbali za namna ya matumizi ya mbolea manunuzi ya bidhaa zao.

1/Post a Comment/Comments

  1. Habari zenu niko Geita naomba mhariri unitafte tafadhali 0743449947

    ReplyDelete

Post a Comment