THE CHOOSEN GENERATION YAIBUKIA VISIWANI ZANZIBAR KUSAIDIA WATOTO WAKIKE MASHULENI


 

Na.Khadija Seif, Michuzi TV


WATOTO wakike Mashuleni bado wanakabiliwa na changamoto ya Taulo za Kike na hata wengine kutumia makaratasi kwa ajili ya kujikinga .


Mkurugenzi wa The choosen generation Nanza Mmbuji akizungumza na Michuzi TV Mara baada ya kutoa Msaada wa Taulo za kike Visiwani Zanzibar ameeleza kwa namna gani amekua akikumbana na changamoto Kwa watoto wakike kukosa Taulo za kike pindi anapokuwa kwenye harakati zake za kusaidia jamii hususani watoto wakike. 


"Nina miaka takribani miwili katika harakati za kusaidia watu wenye uhitaji ikiwemo walemavu,wajane na watoto hasa Mashuleni pamoja na walemavu kutokana na harakati zangu nimegundua uhitaji Mkubwa upo sana kwa watoto Mashuleni hivyo nimeelekeza  nguvu katika kugawa Taulo za Kike kwa wanafunzi Mashuleni Bara na Visiwani kwa kadri ninavyopata nafasi na uwezo."


Nanza amesema Kipindi watoto wanapokua kwenye siku zao Mahudhurio yao yanakua mabaya kutokana na wengi kukosa Taulo za kujikinga na kulazimika kubaki Majumbani na wengine wanatumia vitu ambavyo ni hatarishi kwa Afya zao.   


Pia ameeleza safari yake Kufika Visiwani Zanzibar ni kutokana na harakati zake za kuzunguka Mashuleni hivyo ameguswa kwa dhati kuungana na Kampuni ya consult kuchangia box 5 za Taulo za kike.  

 

 "Nimekua nikitoa Taulo za Kike kama shule ya Kilungule,Baruti na ndio maana nikaweza Kufika Visiwani Zanzibar ili kutoa mchango wangu na kujifunza vingi zaidi,Natoa fungu la kumi kwa ajili ya wenye uhitaji hivyo ningependa Taasisi,Makampuni na hata vikundi kujitokeza kusaidia watoto wakike ili kuwajengea uwezo wa kujiamini."          

.... Mwisho...


2/Post a Comment/Comments

  1. Hongera sana dada kwa kaz nzur sana Mungu azid kukuinua kurudisha tabasamu kwa mtoto wa kike

    ReplyDelete

Post a Comment