NA ISSA MOHAMED
Watanzania wametakiwa
kuacha imani potofu kuhusu ndege aina ya Bundi ambayo amekuwa akihusishwa na
imani za kishirikina huku tafiti za kisayansi zikionesha ndege huyo hausiani
kabisa na imani hizo.
Akizungumza na mwandishi
wa habari hizi mapema leo jijini Dar es salaam Mkuregenzi Mtendaji wa taasisi
ya Mafia Ornithological and research centre Mackubi Joseph amesema Ndege huyo
ana huwezo wa kunusa chembe hai ikiwa mgonjwa anakaribia kufa hivyo
hutumia kama chakula.
Amesema bundi ana
uwezo wa kunusa harufu ya chembe hai zinazokaribia kufa ambapo harufu hiyo
humsukuma kufika katika eneo hilo ambapo wazee wa zamani walimtumia ndege hiyo
kama ishara mbaya endapo nyumba hiyo kuna mgonjwa.
Sambamba na hilo
Mackubi amesema kufuatia mabadiliko ya Tabianchi pamoja na shughuli za binadam
imepeleka zaidi ya makundi hamsini ya ndege wapo hatarini kupokea nchini ikiwa
hatua za makusudi hazijachukuliwa ndege hao ni pamoja na Vocha.
Baadhi ya wakazi
katika kijiji cha simbaulanga wilayani Kibiti mkoani Pwani wamesema kwa miaka
mingi ndege wametumika kama viashiria vya kijadi ila kwa sasa ndege hao
hawaonekani kwa kiasi kikubwa.
Kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa –UN ya mwaka 2020 imeonesha upotevu wa bioanuwai umefikia rekodi ya viwango vya juu ambapo hekta bilioni mbili za ardhi zimepoteza rutuba yake huku zaidi ya aina milioni moja za wanyama na mimea katika sayari dunia viko katika hatari ya kutoweka.
Kweli tumekua tukiamini hivy onakufundishwa hivyo na wazeewetu tubadidilshe mtazamo hasi tuchukue hatua
ReplyDeletePost a Comment