***********
Chama cha hakimili Tanzania (COSOTA),kimesema kimesajili
kazi za wasanii Zaidi ya 500,na wajivunia utendaji wao kazi kupitia mifumo
waliojiwekea.
Hayo yamebainishwa leo mapema Jijini Dar es Salaam na Afisa
uhusiano wa Cosota Anita Jonas wakati
akizungumza na waandishi habari kwenye maonyesho ya 48 ya Biashara Nchini
maarufu Saba Saba .
Anita amesema wao kama Cosota wanajivunia kuwakutanisha
wadau wao husususani wa kazi za Ubunifu na hakimili, pamoja na kuhamasisha
wadau wengine kwenda kwenye Banda lao kusajili kazi na Ubunifu ili kuepusha
wizi na udurufu WA kazi zao
Hata hivyo,Anita amesema Sanaa na Ubunifu ni kazi kama
zilivyo kazi zingine hivyo zinapaswa kulindwa na kuheshimika lakini pia
kumnufanisha muhusika ambaye ametumia jasho lake katika Ubunifu WA kazi zake.
Vilevile Anita ametoa wito kwa jamii Nchini kuhakikisha
wanabadili mtazamo wao kuwa Sanaa ni kazi Rasmi, badala yake wanitumie kazi ya
sanaa kama fursa za kujipatia ajira ya kipato kwa ngazi ya familia au mtu mmoja
mmoja na hatimaye Taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Anita ametoa wito kwa wadau husususani
wale wanatoa mirabaha kwa wasanii waangalie thamani ya kazi za wasanii ili
kuweza kumnufanisha msanii aliyebuni na kufanikisha Kazi husika kwani kwa
kufanya hivyo kutaleta tija kwa msanii husika.
Vilevile,Anita amemshukuru,
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea Kuthamini na kuheshimu
mchango mkubwa WA kazi za wanasanii na wabunifu hivyo amewaomba wadau wengine
kuunga mkono juhudi hizo katika kuleta maendeleo ya Taifa kupitia kazi za Sanaa
na Ubunifu,pia kuwahimiza wasanii kwenda kusajili kazi zao Cosota ili kuepusha
usumbufu WA wizi au udurufu WA kazi zao.
Post a Comment